Home KITAIFA SEKTA YA MADINI IMECHANGIA ASILIMIA 56 MAUZO YA BIDHAA NJE YA NCHI

SEKTA YA MADINI IMECHANGIA ASILIMIA 56 MAUZO YA BIDHAA NJE YA NCHI

Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, amesema kuwa mchango wa Sekta ya Madini katika kuliingizia Taifa fedha za kigeni umekuwa ukiimarika ambapo kwa mwaka 2022 Sekta ya Madini imechangia asilimia 56 ya mauzo yote ya bidhaa zilizouzwa nje ya nchi.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Mbibo leo Julai 5, 2023 alipotembelea wadau mbalimbali wa madini katika banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Aidha, amewataka wadau kuzitumia taasisi zilizo chini ya wizara Tume ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) ili Sekta ya Madini iweze kuchangia zaidi katika Pato la Taifa.

Katika hatua nyingine, Mbibo amezungumza na wadau wa Sekta ya Madini waliopo katika banda hilo ambao wamemweleza huduma wadau wanazotoa, fursa zilizopo katika maeneo ya shughuli zao.

Naibu Katibu Mkuu Mbibo aliongozana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Mussa Budeba na wadau wengine wa Sekta ya Madini.

Previous articleGGML KUTUMIA SHILINGI BILIONI 6 UJENZI UWANJA WA MPIRA GEITA
Next articleWIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAZIDI KUJIZATITI KUTOA ELIMU YA UHIFADHI KWA JAMII

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here