Home KITAIFA SAKATA LA ABIRIA KUPATA ADHA YA USAFIRI LAENDELEA MOROGORO LAFIKISHA SIKU 5,SERIKALI...

SAKATA LA ABIRIA KUPATA ADHA YA USAFIRI LAENDELEA MOROGORO LAFIKISHA SIKU 5,SERIKALI YAOMBWA KUINGILIA KATI

SAKATA LA ABIRIA KUPATA ADHA YA USAFIRI LAENDELEA MOROGORO LAFIKISHA SIKU 5,SERIKALI YAOMBWA KUINGILIA KAT

Sakata la abiria la kupata adha ya usafiri wa kuelekea maeneo mbalimbali ya wilaya za Mkoa wa Morogoro linaendelea kuumiza vichwa vya abiria walio wengi , ni wapi wapate usafiri kuelekea maeneo waendako kutokea mjini Morogoro

Hali hii imedumu kwa siku tano sasa Mkoani humo, ikiwa ni baada ya kutolewa tamko na uongozi wa Wilaya ya Morogoro kuwataka wasafirishaji wa mabasi yaendayo wilayani kuhamia stendi ya Mafiga.

Licha ya abiria na madereva kulalamikia adha wanayopata hivi sasa, Mwenyekiti wa wasafirishaji Aziz Kapilima,anaeleza abiria wanapitia wakati mgumu baadhi yao wakipoteza mizigo yao, akisikitishwa na namna uongozi wa Wilaya unavyoshindwa kukutana na ufumbuzi wa tatizo hilo.

Amesema baadhi ya mabasi yamekuwa yakipakia kwa njia za panya, mengine yakikaa stendi ya Mafiga pasipo abiria, hali ambayo anatoa ombi kwa ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na TAMISEMI kuingilia kati sakata hili.

Stendi ya Mafiga imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5 mjini Morogoro barabara kuu ya Morogoro-Iringa

Previous articleMAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA UHURU KUFANYIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO
Next articleSIMBA SC YAMPA MKONO WA KWAHERI NYOTA MMALAWI PETER BANDA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here