Home KITAIFA RC MAKALLA:TAMASHA LA BULABO MWANZA KUFANYIKA JUNI 13,2023

RC MAKALLA:TAMASHA LA BULABO MWANZA KUFANYIKA JUNI 13,2023

 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA. Amos Makalla leo Juni 7, 2023 wameshiriki kikao cha maandalizi ya Tamasha la Utamaduni la wasukuma (BULABO) ambalo limeandaliwa na kituo cha utamaduni cha Bujora pamoja na Watemi.

Akizungumza na kamati ya maandalizi ya Bulabo kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe.Makalla amewahakikishia kushirikiana nao bega kwa bega ikiwemo upatikanaji haraka wa fedha za kufanikisha tamasha hilo ili liweze kufana zaidi.

“Nawaomba sana tushirikiane vyema kwa kulitangaza ili watu wapate hamasa na kujaa kwa wingi”,amesisitiza CPA Makalla.

Tamasha hili linalenga kuenzi na kudumisha urithi na utamaduni wa Mtanzania hususani wa kabila la Wasukuma na kusheherekea mavuno.

Tamasha hilo linalofanyika kila mwaka lilianza rasmi mwaka 1955 na kwa mwaka huu linatarajiwa kufunguliwa na Chifu Hangaya ambaye ni Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Previous articleWAKUU WA MIKOA WAOMBWA KUHAKIKISHA ELIMU INATOLEWA JUU YA HAKI, ULINZI, USALAMA NA USTAWI WA WAZEE
Next articleWAZIRI UMMY AZINDUA BARAZA JIPYA LA MADAKTARI TANGANYIKA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here