Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge leo April 24, 2023 amefungua Kongamano la Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kongamano hilo limefanyika Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha na kuhudhuriwa na viongozi wa mkoa huo, wanafunzi wa Vyuo, wazee Maarufu, Viongozi wa Dini na watendaji na Watumishi Mbalimbali.
Mhe. Kunenge ametumia wasaa huo kueleza kuwa Kama Taifa tuna kila sababu ya kujivunia namna ambavyo tumeweza kuuenzi na kuulinda Muungano. Ameeleza mataifa makubwa mengi zimeshindwa kulinda Muungano wao.
Amesema kauli mbiu ya mwaka 2023 ya Sherehe za Muungano ni Umoja na mshikamano ndiyo nguzo ya kukuza Uchumi. Amesema kuwa Faida za Umoja ni kubwa kuliko kutengana. Amesesita kila mmoja anawajibu wa kulinda na kuuenzi Muungano.
Amempongeza Serikali kwa mpango mzuri wa maadhimisho ya mwaka 2023. Amesema kuwa watu wengi hawakuwepo wakati wa Muungano hivyo makangamano kama hayo ndyo njia pekee ya kurithishana Muungano.