Home KITAIFA RC AWATAKA WADAU WA ELIMU KUUNGA MKONO UBORESHAJI WA ELIMU NCHINI

RC AWATAKA WADAU WA ELIMU KUUNGA MKONO UBORESHAJI WA ELIMU NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CPA Amos Makala amewataka wadau wa elimu kuunga mkono jitihada za serikali katika kuchangia mpango wa kuchochea na kushawishi wadau wa kushirikiana katika sekta ya elimu GPE Multiplier Grants wenye lengo la kuboresha mazingira ya walimu walioko pembezoni mwa miji,uboreshaji wa Mtaalama mpya wa elimu msingi na kuboresha miundombinu ya Madarasa.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Makala ametoa rai hiyo katika kikao cha wadau wa elimu wa mkoa huo kilichofanyika katimba ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa huyo ambacho kimewakutanisha viongozi mbalimbali akiweo Katibu Tawala wa mkoa huo,Wakuu wa Tasisi za Umma ndani ya mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Tasisi zisizo za Kiserikali pamoja na Wafanyabiashara.

Aidha Makala amewaomba wadau hao kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa wa mpango huo ili kuweza kufanikisha malengo ya kikao ambayo yatapelekea kupata ufadhili kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Dunia.

Katibu tawala mkoa wa mwanza Elikana Balandya amesema mpango wa GEPTeacher Support Programme awamu ya Tatu umelenga katika kuboresha nyumba za walimu na elimu ya awali na msingi hasa katika maeneo ya vijijini pamoja na kutoa motisha kwa walimu

Afisa ufuatiliaji na Tathimini GEP LANES II kutika wizara ya elimu Dkt Nicholaus Gati amesema mpango wa GEP awamu ya tatu ni wa miaka minne kuanzai mwaka 2024 hadi 2027 na utasaidia walimu wanaojitolea kulipwa mishahara.

Aidha dkt Gati amesema mpango huo umeanza mwaka 2014 kwa serikali kupata ufadhili kwa kujenga uwezo stadi kkk tatu kosoma kuandika na kuhesbu.

Previous articleTANZANIA NA ZANZIBAR ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO SEKTA YA MADINI
Next articleKIINI UKOSEFU WA HAKI KWA WALEMAVU CHATAJWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here