Home KITAIFA RASMI MANSPAA YA IRINGA YAFIKIA MAKUBALIANO YA KUINUNUA TIMU YA RUVU SHOOTING,NA...

RASMI MANSPAA YA IRINGA YAFIKIA MAKUBALIANO YA KUINUNUA TIMU YA RUVU SHOOTING,NA KUITWA LIPULI FC

 

Na Dishon Linus

Uongozi wa Manspaa ya Iringa pamoja na wadau wamefikia makubaliano ya kuinunua timu ya Ruvu Shooting iliyoshuka daraja msimu wa 2022/23 ligi kuu Tanzania bara.

Mstahiki meya wa Manspaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amethibitisha hilo leo akizungumza na waandishi wa habari amesema “Ni rasmi Sasa tumekamilisha taratibu zote za kuinunua timu ya Ruvu Shooting yenye makazi yake Pwani na, na ni rasmi pia timu hiyo itaitwa Lipuli FC”

Aidha mstahiki meya ametoa ufafanuzi kuhusu jina la timu hiyo “Lipuli ilikuwa ikishiriki ligi daraja la pili nafasi hiyo itachukuliwa na African wonderez ya mkoani Iringa pia”

Sasa ni rasmi (Wanapaluhengo) Lipuli moja kati ya timu tishio kwenye misimu miwili iliyoshiriki inarejea tena kwenye rada za soka la Tanzania,swali ni je wataweza kupambana kurejea ligi kuu.

Previous articleGST YAKABIDHI KITABU KINACHOONESHA MADINI YAPATIKANAYO TANZANIA KWA MKOA WA DAR ES SALAAM
Next articleREA YAWANEEMESHA WANANCHI KWA KUKAMILISHA KITUO CHA KUPOZA UMEME IFAKARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here