Na Dishon Linus
Klabu ya Real Madrid wamethibitisha kuwa majira haya ya joto wataachana na Rais wao wa muda mrefu wa klabu hiyo Florentino Pelez.
Florentino Pèrez aliirejesha Real Madrid kwenye umaarufu wake kimataifa zaidi,alirejesha fedha za klabu na kuifanya kuwa klabu tajiri duniani. Mpaka sasa Pèrez amejikusanyia mataji 57,vikombe vya Uropa 6.
Kwa mujibu wa jarida la forbes mhandisi Pèrez alichukua Urais mwaka 2000 baada ya kumpiga kwa kura Lorenzo Sanz ambaye alikuwa mkuu wa klabu hiyo wakati huo.
Chini ya usimamizi wake Pèrez amefanikiwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa kama Cristiano Ronaldo, James Rodriguez, Gareth Bale na wengine wengi.
Wakati uongozi wake ukielekea mwishoni anatarajia kufanya umafia mwingine wa usajili kwa kijana wa kifaransa Mbappe dili bado gumu lakini kwake anadai halitamsumbua.