Home KITAIFA RAIS SAMIA KUFUNGUA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA WA LINDI KESHO

RAIS SAMIA KUFUNGUA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA WA LINDI KESHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 19 Septemba 2023 anatarajia kufungua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akisalimia wananchi wa Mtama Mkoani Lindi wakati wa ziara ya Rais Mkoani humo.

Dkt. Mollel ameeleza kuwa hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi baada ya kufunguliwa itaanza kutoa rasmi huduma za wagonjwa wa nje (OPD), Huduma za wagonjwa wa dharura (EMD), huduma za Radiolojia na itamaliza Rufaa zote za huduma za CT Scan baada ya kuanza kutolewa mkoani Lindi hivyo kuwarahisishia wananchi kutosafiri kwenda Dar es Salaam na Mikoa mingine ya jirani.

Previous articleWATUMISHI 7 WA HALMASHAURI YA LIWALE KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO
Next articleMKUU WA MKOA IRINGA AFURAHIA KITABU CHA MADINI YAPATIKANAYO TANZANIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here