Home KITAIFA RAIS SAMIA ATUMA SALAMU KWA MAWAZIRI WA MICHEZO KANDA AFRIKA

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU KWA MAWAZIRI WA MICHEZO KANDA AFRIKA

 

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu kwa njia ya video fupi ambapo amewakaribisha Mawaziri wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV kwenye Mkutano wa kwanza wa Kanda hiyo kufanyika hapa nchini.

“Huu ni mkutano wa kwanza wa kihistoria wa Kanda ya IV kufanyika katika ardhi ya Tanzania tunawakaribisha Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV hapa nchini kwetu ambayo ni Nchi ya amani na ukarimu ikiwa na vivutio vingi vya Utalii Bora Duniani” amesema Rais Dk Samia.

 

Aisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wajumbe wa wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV kuwa Tanzania ipo tayari kuwa Makao Makuu ya Baraza hilo.

Miongoni mwa agenda za mkutano huo ni kuchagua nchi ambayo itakuwa Makao Makuu ya Baraza hilo.

Previous articleTMDA YAPATA HATI SAFI YA UKAGUZI WA CAG
Next articleTANZANIA, INDONESIA KUSHIRIKIANA UENDELEZAJI UCHIMBAJI MADINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here