Home MICHEZO RAIS SAMIA AONGEZA MILIONI 20 KILA GOLI LA YANGA

RAIS SAMIA AONGEZA MILIONI 20 KILA GOLI LA YANGA

 

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza kitita cha Shilingi milioni 20 kwa kila goli timu ya Yanga itakaloshinda katika mechi ya fainali CAFCC.

Rais Samia ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited, Makao Makuu ya Azam Media Limited.

“Ni milioni 20 timu ikitoka na ushindi haitakwenda kafunga mbili kafunga moja hapana yawe magoli yote yameipa timu hii ushindi”

Amesema lakini zaidi ya hapo serikali itatoa ndege kuwapeleka katika mchezo wa fainali “sasa ndege hiyo itabeba wachezaji, mashabiki,na naomba sana wale viongozi wa TFF na mchezo kuwapa moyo kama serikali tunavyofanya” amesema Rais Samia

Previous articleTAKUKURU KAGERA YABAINI MAPUNGUFU KWENYE MIRADI YENYE THAMANI YA BIL.1.5.
Next articleWIZARA YA MADINI YASISITIZA KUENDELEA KUWALEA WACHIMBAJI WADOGO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here