Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na kumteua Prof. Elifas Tozo Bisanda kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Prof Bisanda ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa tume hiyo kwa kipindi cha pili.
Rais Samia Suluhu Hassan Pia amemteua Mhandisi Abdallah Mohamed Mkufunzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Maji.
Uteuzi wa wenyeviti hao umeanza tarehe 05 Mei,2023