Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, amemteua Andrew Massawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na Profesa Ulingeta Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).