Home KITAIFA RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewateua wafuatao:-

i) Amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Miundombinu). Mhandisi Mativila alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

ii) Amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Mhandisi Besta ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (CASSOA).

Mhandisi Besta anachukua nafasi ya Mhandisi Rogatus Hussein Mativila ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

iii) Amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Bw. Anderson Mutatembwa ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu);

na iv) Amemteua Mhandisi Amin Nathaniel Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Uteuzi huu umeanza tarehe 12 Juni, 2023.

Previous articleJAJI MKUU AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI
Next articleSERIKALI KUPITIA WIZARA YA AFYA YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA NAMIBIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here