Home KIMATAIFA RAIS EMMERSON MNANGAGWA AMTEUWA MWANAE KUWA NAIBU WAZIRI WA FEDHA

RAIS EMMERSON MNANGAGWA AMTEUWA MWANAE KUWA NAIBU WAZIRI WA FEDHA

 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amemteuwa mtoto wake wa kiume kuwa naibu waziri wa fedha na kumbakisha Mthuli Ncube kama waziri wa fedha huku akipambana kuokoa uchumi wa nchi hiyo unaodorora.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 yuko chini ya shinikizo la kujenga upya uchumi uliokumbwa na ukosefu wa uwekezaji kutoka nje, ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei na dola ya ndani ambayo imeporomoka kwa asilimia 80 mwaka huu.

Mnangagwa alishinda muhula wa pili baada ya kuwaburuza wapinzani wake mwezi uliopita, ambapo upinzani ulielezea kama “udanganyifu mkubwa” huku kukiwa na ukosoaji kutoka kwa waangalizi wa uchaguzi ambao wanasema uchaguzi huo umeshindwa kukidhi viwango vya kikanda na kimataifa.

Mfanyabiashara wa zamani wa benki, Ncube mwenyewe hajaepushwa kukosolewa baada ya sera zake za kiuchumi kushindwa kuleta ukuaji, huku kukiwa na kushindwa kulipa deni la nje la zaidi ya dola bilioni 17.

Mnangagwa alimteua mwanawe David Mnangagwa kuwa naibu wa Ncube kama sehemu ya mgawo wa vijana katika bunge, huku pia akitangaza Soda Zhemu kuongoza wizara ya madini.

Zhemu alichukua nafasi ya Winston Chitando kama Waziri wa Madini, ambaye aliongoza wizara hiyo tangu Novemba 2017. Alikuwa Waziri wa nishati na maendeleo ya nishati tangu 2020.

Previous articleASHIKILIWA TUKIO LA KUJINYONGA MKOANI MTWARA
Next articleMTWARA JITOKEZENI KUMPOKEA RAIS SAMIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here