Home MICHEZO PUMZI ISIPOKATA HII YANGA SC ITAFANYA MAKUBWA TENA MSIMU HUU 2023/24.

PUMZI ISIPOKATA HII YANGA SC ITAFANYA MAKUBWA TENA MSIMU HUU 2023/24.

 

Na Dishon Linus

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuvuka kuelekea hatua inayofuata ya klabu bingwa baada ya ushindi wa jumala ya magoli saba huku wakiruhusu goli moja katika mchezo leo ambao wao waliupa jina la Max day.

Yanga sc watakutana na Al Merreikh ya Sudan katika mchezo wa mkondo wa pili wa kuitafuta nafasi ya kufuzu makundi ambayo viongozi wa Yanga sc wanadhibitisha kuwa ndio malengo yaoe msimu huu.

Ikumbukwe Yanga sc msimu ulipita aliporomoka hadi shirikisho baada ya kutolewa klabu bingwa na sasa hawataki kurudia makosa.Taarifa njema kwa wapenzi wa soka na mashabiki wa Yanga sc ni juu ya klabu yao inavyocheza kwa kiwango cha juu.

Kwenye mechi walizocheza Yanga sc msimu huu tangu uanze tatizo lilikuwa linaonekana eneo la ushambuliaji lakini kadri siku zinavyokwenda tatizo hilo haionekani tena timu inacheza vizuri na kufunga.

Kwa kiwango wanachokionesha Yanga sc msimu huu kama hawatopunguza kasi yao basi kuna namna mashabiki wakaendeleza furaha za msimu uliopita.

Previous article“VIWATILIFU HUTOLEWA BURE NI MARUFUKU WAKULIMA KUTOA FEDHA” DC MKURANGA
Next articleSERIKALI ITAENDELEA KUMUENZI MAREHEMU MEMBE- MAJALIWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here