Home KITAIFA PROF JANABI ATOA USHAURI KWA KLABU ZA LIGI KUU

PROF JANABI ATOA USHAURI KWA KLABU ZA LIGI KUU

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Profesa Mohammed Janabi amezishauri klabu za Tanzania kuhakikisha zinawapima afya ikiwemo ugonjwa wa moyo wachezaji kabla ya kuwasajili.

Prof Janabi ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 10,2023 jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji na Mwelekeo wa Hospitali hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa Waandishi wa Habari.

Amesema anajua baadhi ya klabu zimekuwa zikisajili wachezaji kwa gharama kubwa bila ya kuangalia afya zao jambo ambalo ni la hatari.

Prof Janabi pia ameshauri wachezaji wanaoshiriki Jogging kuhakikisha wanapima magonjwa ya moyo kabla ya kuanza kukikimbia kwani kutokufanya hivyo ni hatari kwa afya zao.

Prof Janabi pia amelitaka Baraza la Michezo (BMT) Kuweka mikakati ya kuwapima wachezaji wa michezo yote afya ikiwemo ugonjwa wa moyo.

Katika hatua nyingine hospitali hiyo imeanza utaratibu wa kuwatumia waraibu wa dawa za kulevya ambao wameshapona Kwa kuwapa ajira mbalimbali ndani ya hospitali ili wasiweze kurudi tena kutumia dawa hizo.

 

Aidha,Prof, Janabi ameongeza kuwa Mbali na huduma za matibabu ambazo wameendelea kuzitoa Hospitalini hapo wameanzisha utaratibu wa kutoza tozo yapakingi za magari Kwa lengo lakuongeza mapato ya hospitali na kupunguza msongamano wa magari ambayo mengi yameonekana sio ya Wafanyakazi wa hospitali.

 

Previous articleHAKUNA MRADI UTAKAO SIMAMA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA-BITEKO
Next articleMSHINDANO YA GOFU YAMEANZA RASMI MOROGORO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here