Home KITAIFA PPRA KUENDELEA KUWAFUNGIA WAZABUNI WANAOKIUKA SHERIA NA TARATIBU ZA MANUNUZI

PPRA KUENDELEA KUWAFUNGIA WAZABUNI WANAOKIUKA SHERIA NA TARATIBU ZA MANUNUZI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imewafungia baadhi ya wazabuni ambao wamekuwa wakikikiuka mikataba ya ununuzi, kujihusisha na vitendo kinyume na maadili ya sheria za ununuzi wa Umma.

Akizungumza leo Julai 17,2023 jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji na mwelekeo wa wa majukumu ya Mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Eliakim Maswi amesema wamezifungia kampuni kadhaa kufuatia makosa mbalimbali ikiwemo ya udanganyifu wa kugushi nyaraka za taarifa za fedha za benki, na taarifa za malipo ya awali ya benki.

Kadhalika Maswi amesema mikakati iliyopo kwa Mamlaka hiyo kwa sasa ni kuboresha tatizo la ununuuzi wa Umma liwe ni suala la uwazi ili kusiwe na mianya ya rushwa.

“Ukosefu wa uwazi katika mchakato wa ununuuzi wa Umma kunasababisha changamoto za upatikanaji wa taarifa za zabuni ,thamani ya mkataba na kusababisha ukosefu na uaminifu na imani kwa Taasisi za Umma pia hata wananchi wanakosa imani kwa Serikali kutokana na matumizi yasiyoeleweka,

“Waandishi mkiwa watafiti Wazuri mtaona kwamba kuna tatizo kubwa sana kwenye matumizi ya hela za Umma kuna wakati mwingine sisi hatufukirii kusema kwamba ile ni hela ya Umma ilindwe, ndio kwanza wengine wanasema hiyo hela ya Serikali tu sasa nani anapaswa kuilinda ni mimi na wewe” amesema Maswi.

Maswi amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilion 40 kwa PPRA Ili iweze kutekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwemo na kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka hiyo.

Hata hivyo Serikali imekuja na Mfuko mpya wa ununuuzi wa Umma kwa njia ya kielektroniki (NeST) kufuatia Serikali kutumia fedha nyingi zinazoidhinishwa kwenye bajeti kwaajili ya ununuuzi wa bidhaa,kandarasi za ujenzi na huduma kuzingatia matakwa ya Sheria ya ununuuzi wa Umma sura 410.

PPRA ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha sheria ya ununuuzi wa Umma sura namba 410 ambapo malengo ya kuanzishwa kwake ni kuhakikisha upatikanaji wa thamani ya Fedha katika unuzi na ugavi , kuhakikisha uzingatiaji wa haki,ushindani uwazi uendelevu uwajibikaji matumizi mazuri ya Fedha ufanisi na uadilifu katika ununuzi na ugavi.

Previous articleRPC MOROGORO NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MVOMERO WATAKIWA  KUSIMAMIA MIFUMO YA SHERIA KWA ASKARI WANAOENDA KINYUME NA MAADILI
Next articleSERIKALI KUONGEZA UZALISHAJI MBOLEA BORA NCHINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here