Home KITAIFA POLISI MOROGORO WAUNGANISHA MAJESHI YOTE KWENYE MAZOEZI YA PAMOJA

POLISI MOROGORO WAUNGANISHA MAJESHI YOTE KWENYE MAZOEZI YA PAMOJA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limealika majeshi ya ulinzi na usalama Mkoa huo yakiwemo jeshi la wananchi (JWTZ), Magereza, Zimamoto na Uokoaji,Uhamiaji, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) Jeshi la akiba (Mgambo) pamoja na wafanya kazi wa banki ya NMB katika mazoezi ya pamoja.

Akiongea na wanamazoezi hao mara baada ya mazoezi kukamilika kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Hassan Maya amesema, mbali na kujenga afya na kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukizwa, mazoezi haya yanaleta umoja baina ya vyombo vya ulinzi na usalama utakaopelekea kushirikiana kwa pamoja katika kutatua, kuzuia na kupambana na uhalifu.

Kwa upande wake afisa muandamizi Desti Barandagiye kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori (Tawa) amelishukuru jeshi la polisi Morogoro kwa mualiko huo na kuahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwenye mapambano dhidi ya uhalifu.

Aidha meneja wa bank ya NMB tawi la Wami Manispaa ya Morogoro, Harold Lambileki ameliomba Jeshi hilo la polisi kuendeleza zoezi hilo kwani linaleta ushikamano.

Previous articleTANI 13 ZA DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA NA WATUHUMIWA 4983 NCHINI
Next articleAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KUMUUA MWANAFUNZI WA UDOM_ MAGAZETINI LEO JUMAPILI JULAI 30/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here