Home KITAIFA POLISI MKOANI MBEYA WAELEZA SABABU KIFO CHA DEMOGRATIUS MAGUBO

POLISI MKOANI MBEYA WAELEZA SABABU KIFO CHA DEMOGRATIUS MAGUBO

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga, ametoa taarifa ya jeshi la polisi mkoani humo kuwa limeona taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa kampuni ya “Giant Tanzania Printers Ltd” iliyopo Jijini Dar es Salaam ndugu DEOGRATIUS ALPHONCE MAGUBO kilichotokea Juni 21, 2023 akiwa amelala katika nyumba ya kulala wageni iitwayo DICCO INN iliyopo maeneo ya Iyunga Jijini Mbeya kwamba sio cha kawaida.

Ni kwamba Juni 19, 2023 majira ya saa 9:00 usiku, DEOGRATIUS ALPHONCE MAGUBO alifika katika nyumba ya kulala wageni iitwayo DICCO INN akitokea Jijini Dar es Salaam na kuingia kwenye chumba namba 208. Juni 21, 2023 majira ya saa 5:40 asubuhi, zilipokelewa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi Mbeya (Central Police Station) kutoka kwa Meneja wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwamba huko katika nyumba ya kulala wageni iitwayo DICCO INN katika chumba namba 208 kuna mteja aliyetambulika kwa jina laDEOGRATIUS ALPHONCE MAGUBO hajaamka mpaka muda huo.

ACP Benjamin Kuzaga amesema timu ya makachero wa Jeshi la Polisi ikiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Mbeya akiwa ameongozana na kiongozi wa Mtaa huo ilifika eneo la tukio na kuanza kugonga mlango bila mafanikio yoyote hivyo kulazimika kuvunja mlango wa chumba hicho uliokuwa umefungwa kwa ndani na kumkuta DEOGRATIUS ALPHONCE MAGUBO amefariki dunia akiwa amelala kitandani.

Uchunguzi uliofanyika katika chumba hicho mbele ya kiongozi wa Mtaa ulikuta dawa mbalimbali za binadamu, Haloxen 1.5, Haloperidol Injection BP, Valparin Chrono 500, Cough Mixer Syrup pamoja na chupa tupu ya pombe aina ya Grants 750ml, Glass ndani yake ikiwa na vipande vitatu vya limao. Katika
uchunguzi huo uliofanywa na Jeshi la Polisi katika chumba alichokuwa amepanga marehemu umebaini kuwa hakuna kitu kingine kinachotiliwa mashaka.

Aidha, Juni 24, 2023 mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Daktari Mtaalamu wa Upasuaji (Pathologist) wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya mbele ya ndugu wa marehemu na kuchukua sampuli za mwili wa marehemu na kutumwa kwa wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi.

Previous articleAWESO AWAONYA WATENDAJI SEKTA YA MAJI.
Next articleASSEMBLE WATOA MSAADA WA LUNINGA 10 KWA HOSPITALI YA MUHIMBILI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here