Staa wa Afrobeat Olakira kutoka nchini Nigeria, amesema hapoi wala haboi Kwa kuwapa ladha ya ngoma mbili tamu mashabiki wake. Ngoma hizo ni “Ileke” na “Kisses,”.
Akizungumzia kuachia kwa ngoma hizo Olakira anasema zimekuja kukata kiu kwani zitawafurahisha watu wote kwani zimeokwa na kupewa midundo isiyozuilika.
“Ileke,” ni wimbo wangu wa kwanza kwenye hizi mbili ambao unamchanganyiko wa Afrobeat na sauti za kisasa, wimbo huu umetayarishwa na Simba Tagz,
OLAKIRA amesema “Ileke.” inamaana ya umaridadi, kujiamini, na fahari ya kitamaduni. Kwa upande mwingine, “Kisses” nimetayarisha mwenyewe, wimbo huu wa kusisimua unaangazia kina cha mapenzi na matamanio, ni wimbo wa mapenzi unaovutia ambao bila shaka utawaacha wasikilizaji kutamani zaidi”.
Msaani huyo wa Nigeria Mwaka 2020 alitamba na kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘In My Maserati’, Olakira ameendelea kuachia nyimbo nyingi zinazosifika sana na EP, pia akiwa msanii wa kwanza wa Kiafrika katika historia ya ulimwengu, kupata mikataba na kampuni maarufu ya magari ya kifahari ya Italia.