Home KITAIFA NYONGEZA YA KILA MWAKA YA MSHAHARA KUZINGATIWA KUANZIA MWAKA 2023/24

NYONGEZA YA KILA MWAKA YA MSHAHARA KUZINGATIWA KUANZIA MWAKA 2023/24

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema nyongeza ya mshahara ya kila mwaka kwa Watumishi wa Umma ambayo ilikua imesimama kwa muda mrefu itaanza kuzingatiwa mwaka wa fedha 2023/ 24 na kuendelea kwa miaka ijayo.

 

Mhe. Rais Samia amesema hayo Mei Mosi 2023, mkoani Morogoro wakati akihutubia katika siku hiyo ya wafanyakazi iliyoadhimishwa Kitaifa mkaoni hapo.

“Nawahakikishia kuwa, katika uongozi wangu Madaraja yataendelea kupanda, mafao ya wastaafu yatalipwa kwa wakati, kubadilisha kada itazingatiwa na waliondolewa kazini wataendelea kulipwa stahiki zao”, amesisitiza Mhe. Samia.

Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kulipa madai ya wafanyakazi baada ya kumaliza uchambuzi wa madai hayo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mawaziri akiwemo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na viongozi wengine wa Umma na Binafsi pamoja na wanachi wa Mkoa wa Morogoro.

Aidha, sherehe hizo zimepambwa na Maandamo ya wafanyakazi wakiwa na ujumbe mbalimbali wakiwemo wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni Mishahara Bora na Ajira zenye Staha ni nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi.

Previous articleWIZARA KUANZISHA MINADA NA MAONESHO YA MADINI YA VITO NCHINI
Next articleRC MWANZA: WAAJIRI WASIOZINGATIA SHERIA KUWAJIBISHWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here