Home KITAIFA NMB YATOA MIL. 130/- KUDHAMINI BUNGE BONANZA

NMB YATOA MIL. 130/- KUDHAMINI BUNGE BONANZA

 

Benki ya NMB imetoa jumla ya Tsh. Milioni 130 kwaajili ya kudhamini Bunge Bonanza (wabunge, taasisi na watumishi wa Bunge) linalotarajiwa kufanyika Septemba 2 jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari septemba 1, 2023 Bungeni jijini Dodoma Meneja wa NMB Kanda ya kati Janeth Shango amesema tsh. Milioni 90 zimetumika katika ununuzi wa vifaa kama traki suti 1000 , t-shirt , pamoja na kofia 800.

Aidha amesema benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhamasisha michezo ili kujenga afya za watanzania na kuwa na Taifa lenye Watu imara.

Mwenyekiti wa Bunge Bonanza ambaye pia ni mbunge wa jimbo la makete Festo Sanga amesema mgeni rasmi katika Bunge Bonanza ni spika wa Bunge La baraza la wawakilishi Zanzibar Zuberi Ally Maulid na wabunge 10 kutoka Zanzibar pia kutafanyika matembezi yataanza saa kumi na moja alfajiri .

Kauli mbiu katika Bonaza hilo ni Tushiriki Michezo kujenga jamii yenye afya na kuongeza kuwa bonanza hilo litaenda kudumisha mshikano.

‘’Malengo makubwa la mabonanza haya, kama taifa mnavyojua linapambana sana na magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza maka visukari, bipi na magonjwa mengine, sasa kwa shughuli zetu sisi wabunge tukaona ni vyema tukatumia nafasi hii kuweka miili yetu sawa kwa sababu kwas asa taifa linapata shida kwenye magonjwa ambayo siyo yakuambukiza gharama zimkuwa ni kubwa lakini wabung wengi , watumishi wengi na watanzania wengi wamekuwa wakipata shida ,’’

‘’Lakini kubwa zaidi ni kuweka mshikamano kati ya wabunge na watumishi na taasisi tunazofanya nao kazi hapa,ambazo ni mabenki nahususani ijumaa ya kesho ni benki ya NMB, kwahiyo tunawashukuru sana hizo milioni 130 wangeweza kupeleka srhemu nyingine lakini mmetuthamini sana niwakaribishe wananchi wote katika bonanza hilo,’’_alisema

Previous articleDKT. SLAA APIGWA CHINI HADHI YA UBALOZI_ MAGAZETINI LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 02/2023
Next articleDC ILEJE AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA MAPOKEZI YA MWENGE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here