Home KITAIFA NJEZA AZIDI KUZIPAMBANIA BARABARA VIJIJINI.

NJEZA AZIDI KUZIPAMBANIA BARABARA VIJIJINI.

 

Imeelezwa kuwa tarehe 09 Januari, 2023, kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Njombe kilifanyika ambapo moja ya barabara zilizopendekezwa kupandishwa hadhi ni Barabara ya Irambo – Nsonyanga yenye urefu wa Kilomita 22.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri TAMISEMI Deogratius Ndejembi alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njeza alipotaka kujua ni lini Serikali itaipandisha hadhi barabara ya Irambo hadi Nsonyanga ambayo pia inaunganisha Barabara ya Isyonje – Makete hadi Njombe na Barabara kuu ya TANZAM.

“Mheshimiwa Spika, Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) naomba kujibu swali la Mhe. Oran Manase Njeza, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, kama ifuatavyo:- Kamati ya kitaifa ya kupanga Barabara katika hadhi stahiki (NRCC) ilifika Mkoani Mbeya tarehe 24 Februari 2023 na kutembelea barabara zilizoombwa kupandishwa hadhi ikiwemo barabara ya Irambo – Nsonyanga”, Naibu Waziri TAMISEMI Deogratius Ndejembi.

Pia amesema kuwa Mapendekezo ya Kamati yamewasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na yanachambuliwa akisema uchambuzi ukikamilika taarifa
itatolewa.

Endapo barabara hiyo itakidhi vigezo vya kupandishwa hadhi, itakuwa
Barabara ya Mkoa hivyo kuanza kuhudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Mbunge Njeza amekuwa akizipigia chapuo barabara zake za Mbeya vijijini ili kuona zinajengwa na kuboreshwa ili kuwasaidia wananchi wake hasa wakulima ambao ndio wengi jimboni Mbeya vijijini.

Previous articleWADANGANYA , WATUMIA VYETI FEKI KUOMBA AJIRA _MAGAZETINI LEO JUMANNE JUNE 06/2023
Next article“NHIF YAELEKEZWA KUTOA HUDUMA MPAKA NGAZI YA ZAHANATI NA WAF- MHE GODWIN MOLLEL

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here