Home MICHEZO NI YAPI MALENGO YA YANGA SC MSIMU UJAO 2023/2024

NI YAPI MALENGO YA YANGA SC MSIMU UJAO 2023/2024

 

Na Dishon Linus

Yanga Sc msimu uliomalizika wa 2022/2023 timu ilifanikiwa unaweza sema kwa asilimia zaidi ya 90% kwani kwenye mashindano yote aliyopata nafasi ya kushiriki basi timu iliweza kuonesha matokeo chanya japo kimataifa kwenye klabu bingwa waliondoshwa na kuangukia kombe la shirikisho ambako walifika fainali.

Hapa nyumbani Tanzania Yanga sc ilibeba makombe yote yanayotambulika na shirikisho la soka Tanzania (TFF) na ikiwa ndio timu iliyofanikiwa zaidi ukanda huu wa Afrika mashariki.

Baadhi ya walichagiza mafanikio hayo wengiwao wameondoka kwenye timu benchi la ufundi likiongozwa na Nabi na msaidizi wake Kaze na baadhi ya wachezaji kama mfungaji bora wa timu hiyo Mayele na hivi sasa wako na mwalimu mpya na baadhi ya wachezaji wapya.

Sasa nini malengo ya Yanga sc msimu mpya 2023/2024, Makamu wa Rais Arafat Haji anasema “Sisi malengo yetu yapo pale kuhakikisha wananchi wanaendelea kutamba na kuwa na furaha, lakini tunafahamu msimu uliopita tumebeba mataji matatu adhima na malengo yetu ni kuhakikisha makombe yanabaki makao makuu ya mataji Jangwani.”-

“Lakini pia msimu uliopita tumetoka kucheza fainali ya Kombe la shirikisho Afrika na msimu huu tutahakikisha tunafika mbali zaidi ikiwezekana kuweka historia nyingine ya kucheza fainali ya Klabu bingwa Afrika”-

Mpaka sasa Yanga sc wamecheza mchezo mmoja tu wakirafiki tangu timu ianze maandalizi ya msimu mpya nayo ni mechi ya siku ya mwananchi dhidi ya kaizer chief na kufanikiwa kushinda gori moja la Kennedy Musonda.

Previous articleMKUU WA CHUO CHA MAFUNZO YA UFUGAJI NYUKI TABORA – BTI AWEKA BAYANA MATUNDA YA UJIO WA WATU 10 KUTOKA AFRIKA KUSINI
Next articleTANI 700 ZA SALFA ZIMEPOKELEWA PWANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here