Papa Francis ameonya kuhusu watu wa Italia kuishi kwa ukaribu zaidi na mbwa na paka kiasi cha kuchukua nafasi ya watoto kwenye kaya.
Akiwa mjini Roma Papa Francis anasema hali hiyo imetokana na ugumu wa kuanzisha familia nchini humo kutokana na gharama kubwa za maisha na ukosefu wa ajira na mishahara ya kutosheleza mahitaji.
Papa Francis alisimulia namna mwanamke mmoja alipofunga begi lake na kumuomba ambariki mtoto wake na badala yake hakuwa mtoto wa kuzaa bali mbwa mdogo.
“Nilipoteza uvumilivu wangu na kumwambia: kuna watoto wengi ambao wana njaa na unaniletea mbwa?”- aliongeza na kusababisha makofi kutoka kwenye umati uliokuwa ukimsikiliza.
Italia ambayo mara nyingi huitwa nchi ya Vitanda vitupu inatajwa kuwa inaweza kupoteza karibu theluthi moja ha wakazi wake ifikapo 2050 kutokana na kuongezeka mara tatu zaidi ya wazee walio na miaka zaidi ya 100 huku idadi ya wanaozaliwa ikishuka kwa takribani vizazi 400,000.