Kuelekea siku ya maonesho ya Nanenane yanayofanyika kila ifikapo Augosti 8 kila mwaka, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema kuwa maonesho ya mwaka huu yametengewa siku nne ambazo zitakuwa maalumu kwa uhamasishaji wa vitu mbalimbali kama vile utalii na uhifadhi wa mazingira,kuhamasisha ulaji wa korosho,ulaji wa vyakula vya asili pamoja na kuhamasisha ulaji wa vyakula vya bidhaa ya viumbe wa baharini na mifugo.
Kanali Abbas ameongeza kuwa mpaka sasa tayari miundombinu imekamilika kwa eneo la Ngongo mkoani Lindi, na sherehe za Nanenane Kanda ya Kusini zinatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500 sawa na ongezeko la 36% ambapo ni tofauti na mwaka jana maonesho yalihudhuriwa na watu 366.