Naibu waziri wa maji Mhandisi Mary Prisca Mahundi amewata vijana wa kike kuamka pamoja na kujitoa katika unyonge ili kuweza kupambania ndoto na kufikia malengo .
Amesema hayo mkoani Morogoro katika usiku wa tuzo za wanawake wapambanaji zilizoandaliwa na taasisi ta ladies talk zenye lengo la kuwainua wanawake katika nyanja mbalimbali.
Kwa upande wake mbunge wa ulanga Salim Alaudin Hasham amewaasa vijana kike kujipambanua kwa kufanya kazi yoyote na kuacha kufanya shughuli walizozizoea kama uuzaji wa nguo ,mikoba pamoja na Makeup.