Home KITAIFA NAIBU SPIKA MHE. ZUNGU MGENI RASMI MAONESHO YA WIZARA YA UTAMADUNI

NAIBU SPIKA MHE. ZUNGU MGENI RASMI MAONESHO YA WIZARA YA UTAMADUNI

Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dodoma

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu anatarajiwa kufungua maonesho ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na taasisi zake yatakayofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 5-6, 2023 katika viwanja vya Bungeni jijini Dodoma.

Akikagua maandalizi mabanda yatakayotumika kwenye maonesho hayo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu amesema wizara hiyo ambayo ni nguvu shawishi ya Serikali itatoa fursa kwa Wabunge kujifunza na kuona kwa vitendo kazi zinazofanywa na Wizara hiyo kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti yake Juni 6, 2023.

Bw. Saidi Yakubu anawakaribisha Waheshimiwa Wabunge na wageni wote wa Bunge kutembelea mabanda ya Wizara hiyo pamoja na taasisi zake ili kupata huduma zinazotolewa na wizarani hapo na taasisi zake.

Aidha, Wizara hiyo itatumia fursa hiyo kutoa baadhi ya vifaa vya michezo kwa waheshimiwa Wabunge pamoja na vitendea kazi vingine ambayo vinatumika kurahisisha utendaji kazi wao wa kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.

Previous articleMAGUNIA 731 YA BANGI YAKAMATWA ARUSHA_ MAGAZETINI LEO JUMATATU JUNI 05/2023
Next articleWANASHERIA WAMEIPOTOSHA SERIKALI, MAWAZIRI KUHUSU MCHAKATO KAMPUNI YA SARUJI YA TWIGA KUNUNUA HISA ZA TANGA CEMENT-JAJI MIHAYO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here