Home KITAIFA NAIBU CAG ZANZIBAR AAPISHWA

NAIBU CAG ZANZIBAR AAPISHWA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amemwapisha Dkt .Said Khamis Juma kuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hafla hiyo ya uapisho imefanyika Ikulu Zanzibar kabla ya kuanza kikao cha Tume ya Mipango.

Rais Dk. Mwinyi ameendelea kuweka msisitizo katika kuimarisha utawala bora, uwazi, na uwajibikaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, lengo likiwa ni kuhakikisha ufanisi wa matumizi ya rasilimali za umma.

Dkt.Said Khamis Juma Naibu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali  atamsaidia Dkt.Othman Abbas Ali Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar kuhakikisha  matumizi ya fedha za umma yanafanyika kwa uwazi, ufanisi, na kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo.

Previous articleMFUKO WA DUNIA KUENDELEA KUFADHILI AFUA ZA KUPAMBANA NA UKIMWI, MALARIA NA KIFUA KIKUU NCHINI
Next articleTANTRADE NA UCSAF KUTOA HUDUMA YA MAWASILIANO (WIRELESS INTERNET-Wifi) ) KATIKA UWANJA WA MAONESHO YA SABASABA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here