Home KITAIFA NACTIVET YASIMAMISHA MAFUNZO CHUO CHA MBEYA TRAINING..DC MALISA AAGIZA KUFANYIWA UHAKIKI VYUO...

NACTIVET YASIMAMISHA MAFUNZO CHUO CHA MBEYA TRAINING..DC MALISA AAGIZA KUFANYIWA UHAKIKI VYUO VYOTE WILAYA YA MBEYA

Wazazi, wanafunzi na wahitimu wa chuo cha Mbeya Training wameiomba serikali iwasaidie kurudishiwa stahiki zao mara baada ya kubainika kozi waliyokuwa wanasoma chuoni hapo haitambuliki na Balaza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTIVET).

Ombi hilo wamelitoa mbele ya mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa na Meneja wa NACTIVET Kanda Joha Fugutilo mara baada ya kuagiza chuo hicho kusimamisha mafunzo kutokana na kukiuka masharti ya uendeshaji huku Mhe. Malisa akiagiza NACTIVET kufanya uhakiki wa vyuo vilivyopo wilayani Mbeya.

Katibu mtendaji wa NACTIVET Tanzania kupitia kwa Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Joha Fugutilo mbali na kuagiza chuo hicho kusimamisha utoaji wa mafunzo lakini pia amesema mmiliki asipotoa maelezo ndani ya siku saba chuo hilo kitafutiwa usajili wake.

Kwa upande wa wanafunzi wamedai wameiomba serikali kusaidia kupata suluhu ya jambo hilo kutokana na wengi wao kupoteza muda wakiwa chuoni hapo na hasara Iliyojitokeza.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno Malisa ameagiza vyuo vyote vilivyoko wilayani kwake kuhakikiwa usajili ili kuepusha udanganyifu kama uliojitokeza.

Mmiliki wa chuo hiki Joseph Asajile amekataa kuzungumzia tuhuma hizi zinazomkabili.

Previous articleVIONGOZI WA SERIKALI WASIUMBULIWE HADHARANI – MLAO
Next articleDKT. BITEKO AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA BIASHARA WA KOREA KUSINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here