Baada ya siku chache Dkt Mwakyembe kuyataja baadhi ya Mashirika ya kiraia kujihisisha na Shughuli za maswala ya ndoa za Jinsia moja (Ushoga) leo Baraza la Taifa la NGO’s limetoa tamko lao juu ya hatua ambazo watazichukua juu ya Tuhuma Hizo
Akiongea na Waandishi wa habari Dar es Salaam Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Lilian Badi amesema kuwa wamefanyika kikao cha dharura cha Kamati tendaji kujadili, kuchangamua na kuweka maazimio ya utekelezaji kuhusiana na swala hilo.
Pia Lilian ameeleza Baraza limefanya mawasiliano na Mashirika yote ambayo yamehusishwa kwenye hutuma hizo, ikiwa ni maandalizi yake ya kufanya uchunguzi pamoja na mahojiano ya kina kwenye Baraza la maadili ya Kamati hiyo.
Pia Baraza ilo limeomba kukutana na Kamati ya Daktari Mwakyembe ili kupata taarifa yao na kuwaeleza namna watashughulilia swala hilo kama viongozi wa sekta ya NGO’s.
Katika hatua hiyo Baraza la NGO’s limewataka watanzania kuziona tuhuma alizotoa Dkt Mwakyembe ni tuhuma za swala mtambuka na sio NGO’s pekeake ila hata wadau ambao hawakutajwa kwenye tuhuma hizo hivyo busara zitumike kwenye kushughulikia swala hilo.