Home KITAIFA MWENYEVITI WA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA WASIOWAJIBIKA KWA WANANCHI HAWAHITAJIKI WASIPEWE NAFASI...

MWENYEVITI WA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA WASIOWAJIBIKA KWA WANANCHI HAWAHITAJIKI WASIPEWE NAFASI MWAKANI- KATIBU WA NEC ORGANIZASHENI TAIFA HAJI

Na Scolastica Msewa, Kibaha

Katibu wa NEC. Organaizesheni Taifa Issa Haji Ussi Gavu amesema CCM hakihitaji Viongozi wa mitaa, vitongoji na vijiji wasiowajibika kwa Wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji mwakani wasipewe nafasi za kuongoza hatuwahitaji ndani ya CCM.

Amesema hayo wakati akihutubia Wazee wa CCM na Jumuhia ya Wazazi mkoa wa Pwani kwenye mkutano alipofika Kibaha mkoani Pwani kuzungumza na Wazee wa mkoa mzima wa Pwani.

Haji alisema Viongozi ambao hawawajibiki ipasavyo kwa wanaowaongoza, viongozi hao hatuwahitaji ndani ya CCM Bali tunataka kumuona Mwenyekiti wa kijiji, Mwenyekiti wa kitongoji, Mwenyekiti wa mtaa aliyetayari kuhangaika na mambo ya watu anaowaongoza.

Tumepata taarifa wapo baadhi ya Wenyeviti wetu wa vijiji, vitongoji na mitaa wanashindwa kukithi matakwa ya Katiba na kanuni yaani Viongozi wasiowajibika kwa Wananchi hivyo katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji mwakani wasipewe nafasi”

“Kama Mwenyekiti wetu anashindwa kusitisha vikao wala mikutano ya kuelezea mapato na matumizi ya fedha Mwenyekiti huyo achaneni nae, tafuteni Mwenyekiti wa kijiji, mtaa au kitongoji atakayesimama mbele ya watu anaowaongoza ambaye wao wenyewe watakiri na kusema huyu ni kiongozi kweli”

“Maana hatuna sababu ya kupanda Mlima wakati kichuguu kipo tafuteni watu wanaouzika kwa kukubalika watakaokisaidia Chama chetu, tafuteni watu nafasi ya uongozi watakao kwenda kusimama kuhangaika na mambo ya watu anaowaongoza”

“Natumepata taarifa wapo wabunge, Madiwani wanaoangaika kupanga safi za viongozi wa vitongoji, vijiji na mitaa kwa madhumuni ya kwamba wawasaidie kwenye kura za maoni mwaka 2025 ili wasipoteze kura zao”

“Tunamuhitaji Diwani, Mbunge apambane Wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa ndani ya Kata yake na ndani jimbo lake washinde kwa kura za walio wengi au Mbunge au Diwani umepoteza mitaa, vijiji, vitongoji wewe kwa nafasi yako unashida kwenye chaguzi hizo kwani viongozi hao ndio daraja baina yako wewe na watu hao unaowaongoza kama daraja limevunjika hauna namna ya kufika ng’ambo ya pili”

“Tukuhakikishieni sisi kama CCM kwa haki kabisa kuona kwamba tunajipunguzia mashaka ya watu wasiokuwa na sofa au kuhangaika na mambo ya watu maana tunahitaji viongozi watakaokuwa tayari kwenda kuhangaika na mambo ya watu anaowaongoza”

Aidha amewataka wa viongozi wa CCM na wanaCCM kufanya vikao vya kikatiba ilikujua kero na changamoto zinazowakabili Wananchi wanaowaongoza na kuzitafutia ufumbuzi.

Alisema kumekuwa na tatizo kubwa la viongozi kutotimiza vikao vya kikatiba na vya kikanuni vya ndani ya CCM.

Alisema kwa mujibu wa ibada 124 ya Katiba ya CCM Wazee ni taasisi na wanatakiwa kuhudhuria vikao harali vya ndani ya CCM.

“Rudini mkasome kanumi toleo la mwaka 2019 kuanzia ibada ya tatu ambayo inaelezea madhumuni na muhimu wa Baraza la Wazee kwa ngazi ya msingi imeanzishwa Baraza hili la Wazee kwa lengo la kurithisha tabia Njema kwa taifa letu”

Limeanzishwa Baraza la Wazee kwa madhumuni ya viongozi wa CCM kuweza kurithisha Mila na desturi zetu kwa taifa hili na ni chombo Cha kuwaunganisha Wazee wote kwa itikadi ya CCM kwahiyo niwasihi na niwaombe msione tabu wala msione shida kurudi kwenye ngazi husika iwe ngazi ya Wilaya, Kata, au ngazi ya tawi kwenda kushauri kwenye ngazi husika ili mambo yafike yaende vizuri.

“Mkichelea kusema au kushauri mtakuwa hamkitendei haki Chama chetu, taifa na hamuitendei haki nafasi na fursa mliyopewa na Katiba yetu maana nyinyi ni washauri mambo yakienda vibaya hamna namna ya kukataa lawama hizo, mtabeba msalaba huo wa kutokushauri, kutoongoza na kutokutupa maelekezo ili mambo yanyooke” alisema Haji.

“Chama hiki ni chama cha Watanzania wa tabaka zote awe mnyonge au tajiri, awe mrefu awe mfupi, awe mweupe awe mweusi mategemeo yake na kimbilio lake ndani ya Taifa hili ni CCM nyinyi mmepewa nafasi, sehemu ya kwenda kusimamia utekelezaji na miongozo sahihi katika kupata viongozi wazuri wa taifa letu” alisema Haji.

Aliongeza kuwa “Ukisoma ibala ya 76-78 ya Katiba ya CCM toleo la mwaka 2022 imetuelekeza kuwa Wazee ndio vikao vya mwisho vya uteuzi wa Wenyeviti katika nafasi ya vitongoji, vijiji na mitaa niwaombe sana mwende mkasimamie haki itendeke na mtumie nafasi ya kushauri kuhakikisha kwamba haki inatendeka na waliopo madarakani wanatimiza wajibu wao”

Naye Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifafanua changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na Wazee hao amewaomba watoe ushirikiano wa kuzingatia sheria na kanuni za Nchi katika kumaliza migogoro ya Wakulima na wafugaji mkoa wa Pwani ikiwa ni pamoja na kuunga mkono kuanzishwa kwa Ranchi ndogo za mifugo mkoani humo.

Lakini pia Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani aliwata Wazee kuzingatia malezi Bora kwa watoto wao ili kuepusha mkoa huo na taifa kwa ujumla kizazi kisicho na matendo yasiyo na maadili yanayowaingiza kwenye makundi ya uharifu kama panda road.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Mafia Hamisi Mbangu ameomba kuhimarishwa kwa usafiri wa anga na usafiri wa kwenye maji kwenda na kurudi katika kisiwa cha Mafia.

Previous articleHUYU MWANAMKE ANANIPA MAPENZI HADI NACHANGANYIKIWA
Next articleMAMA , MTOTO WAUAWA KINYAMA ,WAHUSIKA WAONDOKA NA KICHWA_ MAGAZETINI LEO JUMAPILI NOVEMBA 26/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here