Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linaendelea na uchunguzi kufuatia kifo cha mwenyekiti wa simba Benson Mwakasanga (48) tawi Mchombe kata ya Mngeta halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro aliyeuawa kwa kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana.
Kaimu kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro Hassan Omary amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema tukio hilo limetokea julai 25 ,2023 akiwa shambani kwake .
Naye Mwenyekiti wa simba matawi ya Morogoro Saidi Mkwinda ameeleza namna uongozi wa matawi ulivyosikitishwa kutokea kwa tukio hilo.