Kufuatia tukio la kifo cha Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma Nusura Hassan Abbdallah kuendelea kujadiliwa katika mitandao ya kijamii na watu mbalimbali wakitaka uchunguzi wa kina kufanyika ili ukweli kupatikana,Jambo TV imefanya mahojiano maalumu na Mwenyekiti wa Kijiji Cha Uchira Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro Julius Mkojera inapoelezwa kuwa ndipo alipofia Binti huyo,kutaka kujua ukweli wa tukio hilo.
Akiongea na Jambo TV Mei 7/2023 Mkojera amesema kuwa tukio hilo hajaliona na halikutokea katika kijiji chake bali amekuwa akisikia uvumi huo na ameendelea kuchunguza ili kupata undani wa taarifa ya uwepo wa msiba huo bila mafanikio
“Hakuna kilichotokea katika Kijiji cha Uchira na hao watu waliotoa huo umbea naomba wakamatwe kuna mwandishi mwingine alinipigia nikamwambia kuwa acha nichunguze nilipoanza kuchunguza kila mtu ana shangaa hakuna kitu kama hicho”.
“Hata leo kule Kanisani nimeuliza kuhusu hilo tukio hakuna anaye lifahamu,Hospitali ya Faraja ndio inayoweza kueleza kama walipokea mgonjwa kutoka eneo hili ila kwakweli tukio hilo halijatambulika hapa kijijini” alifafanua Mkojera.
Awali Diwani wa Kata ya Kirua Vunjo Kusini Bw.Meela akiongea na Jambo Tv alisema kuwa taarifa anazo fahamu ni kuwa Binti huyo hakufia kwenye Kata yake.
“Baada yaa kuangalia na kuchunguza huyo Binti hakufia kwenye Kata yangu ya Kirua Vunjo Kusini .