Home KITAIFA MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI WENYE UJAZO WA LITA LAKI...

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI WENYE UJAZO WA LITA LAKI TANO WILAYANI ILEJE

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdallah Shaibu akiongea na wananchi wa Ileje mara baada ya kuzindua mradi wa maji kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Mheshimiwa Farida Mgomi Septemba 06, 2023 

Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa leo Septemba 6, 2023 umeweka jiwe la msingi kwenye tenki la mradi wa maji lenye ujazo wa lita laki tano(500000).

Mradi huo unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 1 Kwa ajili ya kusambaza maji katika kijiji cha Ntembo kata ya Chitete wilayani.

Ndugu Abdala Shaibu kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ameagiza kumpelekea maji mzee Folo Sinkonde ambaye ametoa eneo kwa ajili ya kujenga tenki la maji.

“Hakikisheni mradi huo unawanufaisha wananchi wote wa kijiji cha Ntembo na kuweka kwenye taasisi ili dhamira ya Rais Samia kumtua ndo kichwani inatimia ,”amesema Ndugu Abdala Shaib

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi amesema, mradi huo utakuwa tunu kwa wananchi kwani ni moja ya miradi wilayani ambayo utaenda kutatua changamoto ya kumtua ndoo mwanamke kichwani na maelekezo ya kumwekea mzee maji aliyetoa eneo litatekelezwa kufikia Septemba 30, mwaka huu.

Previous articleREA KUIPATIA UMEME SHULE YA CHIFU HANGAYA ILIYOKO MAGU
Next articleKATIBU MKUU KIONGOZI ATEMBELEA MRADI WA JNHPP, ASEMA WATANZANIA WANAHITAJI UMEME

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here