Home KITAIFA MWAUWASA WAPEWA WIKI 6 KUANZA KUWASAMBAZIA MAJI WANANCHI

MWAUWASA WAPEWA WIKI 6 KUANZA KUWASAMBAZIA MAJI WANANCHI

 

Waziri wa maji Mhe. Jumaa Aweso ametoa wiki 6 kwa Mamlaka ya maji Mkoa wa Mwanza ( MWAUWASA ) kuanza kusambaza maji kwa wakazi wa Busweru Wilayani Ilemela.


Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango kufuatia ziara yake katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza , Waziri wa maji amesema Serikali imekwisha toa sh. Milioni 500 za ukamilishaji wa Tenki hilo litakalochukua lita Mil.3 za maji Hivyo amewataka mwauwasa kuanza kusambaza maji kwa wananchi ndani ya wiki 6.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemtaka Waziri wa maji Jumaa Aweso kuhakikisha miradi yote ya maji inayotekelezwa Wilayani Ilemela inakamilika kwa wakati ili ianze kutoa huduma kwa wananchi huku akimtaka kuwawajibisha watendaji wote watakaokwamisha kukamilika kwa miradi hiyo.

Aidha akiwa Wilayani Magu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Fiderica Myovera kutoa mili. 18 kwa ajili ujenzi wa uzio kwenye kituo cha afya Kisesa ili kuimarisha hali ya usalama katika kituo hicho.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mkoani Mwanza (MWAUWASA) Eng. Leonard Msenyele amemuhakikishia makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Isdor Mpango kusimamia ujenzi wa miradi yote mipya ya maji inayotekelezwa Mkoani humo kwa viwango na ubora ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi.

Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dr. Angelina Mabula ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo hilo.

Previous articleBABA MZAZI ATUHUMIWA KUMLAWITI MWANAE WA MWAKA NA MIEZI 7
Next articleWATU 400 KUFANYIWA UPASUAJI WA MTOTO WA JICHO MBARALI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here