Home KITAIFA MWANRI: WAKULIMA WAKIFUATA KANUNI BORA ZA KILIMO CHA ZAO LA PAMBA WATAPATA...

MWANRI: WAKULIMA WAKIFUATA KANUNI BORA ZA KILIMO CHA ZAO LA PAMBA WATAPATA UZALISHAJI WENYE TIJA

Balozi wa zao la Pamba nchini Agrey Mwanri amewataka maafisa Ugani wilayani Rorya Mkoani Mara kwenda kuwasimamia wakulima kuondokana na Tabia ya kilimo cha kurusha mbegu kwani kilimo cha namna hiyo kimepitwa na wakati badala yake kulima zao hilo kwa kufata kanuni Bora zinazotakiwa.

Kauli hiyo ameitoa Balozi wa zao la Pamba Agrey Mwanri katika kikao Kazi baina yake na maafisa Ugani wilayani Rorya Mkoani Mara .

Mwanri amesema wakulima endapo wanatafuata kanuni Bora za kilimo zitawasaidia kuwa na uzalishaji wenye tija ambao utawasaidia kuwakomboa katika kilimo cha zao hilo.

Awali akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Rorya Juma Chikoka amewataka maafisa Ugani hao kwenda kufikisha Elimu hiyo kwa wakulima ili kuhakikisha zao hilo linakuwa na tija kwa wakulima bankujivunia inayotokea ajenda ya kilimo cha zao la pamba.

“Twendeni kupushi hii ajenda ya kilimo hasa kwenye zao la Pamba ili inapokuja kuhusu kilimo wakulima wetu waione Pamba ndio mkombozi wagonjwa Wana Rorya.

Previous articleVIJANA WATAKIWA KUKUZA UCHUMI MAPEMA ILI KUJENGA FAMILIA ZAO
Next article“MSIKUBALI UPOTOSHAJI WA WAZUSHI, BANDARI HAIUZWI” MBUNGE DKT. CHAYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here