Home KITAIFA MWALIMU, MLINZI KORTINI KWA KUMJERUHI MWANAFUNZI MBEYA

MWALIMU, MLINZI KORTINI KWA KUMJERUHI MWANAFUNZI MBEYA

 

NA JOSEA SINKALA.

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Rohilah iliyopo katika Kata ya Utengule Usongwe Mbalizi Emmanuel Petro Kamili (29), aliyekuwa akituhumiwa kumpiga na kumjeruhi mwanafunzi wake amefikishwa mahakamani pamoja na mlinzi wa shule hiyo na kusomewa shtaka la kusababisha majeraha makubwa kwa mwanafunzi huyo.

 

Akisoma hati ya mashtaka mahakamani mbele ya Hakimu mkazi Mkuu katika mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya Paul Ntumo, Mwendesha mashtaka wa Serikali Emelda Aluko amesema washtakiwa walitenda kosa hilo Februali 12 mwaka huu.

Amesema siku ya tukio Mwalimu Emmanuel Petro na mlinzi wa Shule hiyo Haruni Isaya Kerupe (30) wote wakazi wa Iwala Mbalizi walishirikiana kumpiga mwanafunzi aitwaye Rawlance Mwangake mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule yabupili Rohila ambaye walikuwa wakimtuhumu kudokoa maandazi kwenye duka shuleni hapo hali iliyomsababishia maumivu makali kosa ambalo ni kinyume na kifungu namba 225 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 ya mwaka wa jana 2022.

 

Mshtakiwa wa kwanza Mwalimu Emmanuel amekana kutenda kosa hilo mbele ya mahakama huku ukiri wa kukubali au kukana kosa hilo ukibaki kwa mshtakiwa wa pili Haruni Kerupe ambaye hakuwepo mahakamani badala yake aliwakilishwa na mdhamini wake akidaiwa hajafika mahakamani kutokana na kuuguza mmoja wa wazazi wake.

 

Hata hivyo Jamuhuri kupitia mwendesha mashtaka Emelda Aluko inasema upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo kuahidi kuwasilisha ushahidi wake mahakamani ili kuthibitisha tuhuma dhidi ya wawili hao kumpiga na kumjeruhi mwanafunzi wao.

Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya Paul Ntumo ameahirisha kesi hiyo hadi hapo baadaye kwa ajili ya uchambuzi hoja za awali kisha kuanza kusikiliza shauri hilo la jinai na mshtakiwa wa kwanza ameachiwa huru kwa dhamana..

Previous articlePOLISI YATOA ELIMU YA UKATILI NA UNYANYASAJI MBEYA
Next articleSAKATA LA TANGA CEMENT BADO LACHEMKA _ MAGAZETINI LEO JUMANNE MEI 09/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here