Home KITAIFA MWALIMU MAGANGA : NINA AJIRA YA KUDUMU CWT

MWALIMU MAGANGA : NINA AJIRA YA KUDUMU CWT

Mara baada ya taarifa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliyotolewa na Mkurugenzi Elihuruma Mabelya ikielezea kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu nchini (CWT), Mwalimu Josephat Maganga, ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi Tandika iliyopoko Wilayani Temeke, kumeibuka sintofahamu ya iwapo maamuzi hayo ya kusimamishwa kazi yatamuondolea sifa Mwalimu Japheth Maganga ya kukiongoza Chama cha Walimu Nchini (CWT)

Mara baada ya taarifa hiyo kutolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke hapo jana Alhamisi Desemba 07, 2023 baadhi ya waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 08, 2023 wakafunga safari kumtafuta Mwalimu Japheth Maganga kupata kauli yake baada ya kusimamishwa kazi na endapo kusimamishwa huko kutamfanya akose sifa ya kuwa Katibu Mkuu wa CWT, katika mahojiano maalum hayo baina ya waandishi wa habari na Mwalimu Maganga ikiwemo kuhusu hatma yake katika nafasi ya uongozi wake ndani ya CWT Mwalimu Maganga amesema yeye ana mkataba wa kudumu wa ajira ya CWT hivyo ni mtumishi wa CWT na hata wakati anagombea nafasi aliyonayo hivi sasa alitokea makao makuu ya CWT kama Mhasibu hivyo kwa muujibu wa katiba ya CWT toleo la mwaka 2014 bado anazo sifa za kuwa mwanachama wa CWT hivyo uhalali wa yeye kuendelea na nafasi yake ya sasa hautakoma baada ya kusimamishwa kazi.

“Niliajiriwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kama mhasibu tarehe 01 Januari, mwaka 2018” alikaririwa Mwalimu Maganga

Baada ya hapo, Mwalimu Maganga amesema, aligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT akitokea idara ya uhasibu CWT– Makao Makuu na si Halmashauri kama ambavyo wengi wanadhani,

Mwalimu Maganga ameongeza kuwa, kwa mujibu wa katiba ya CWT toleo la mwaka 2014 ana haki ya kugombea nafasi ya yoyote ndani ya CWT.

“Kwa mujibu wa ibara ya 6.4 ya Katiba ya CWT ya mwaka 2014 mimi ni wanachama maalum na nina haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya CWT, ibara ya 30 (e) ya katiba ya inathibitisha hilo”.

Itakumbukwa, kupitia mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) tarehe 16 Desemba, 2022 ulimthibitisha kuwa Katibu Mkuu wa CWT.

Mwalimu Maganga amehitimisha mahojiano kwa kusema kuwa, yeye bado anayo haki ya kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa CWT na haki hiyo amepewa kikatiba.

“Nina haki ya kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa CWT kwa mujibu wa katiba ya cwt ibara ya 30 (e) toleo la mwaka 2014”

Hata hivyo, Jambo TV imefanikiwa kuona nakala ya mkataba unoatambulika kama mkataba wa kudumu wa ajira ya kati ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) na Mwalimu Japhet Maganga uliosainiwa tarehe 02 Januari, mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa hapo jana Alhamis Desemba 07, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya imeeleza kuwa, Mwalimu Maganga amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za utoro kazini na kukaidi au kukataa maelekezo halali ya Viongozi.

Previous articleWADAIWA SUGU DODOMA WATOLEWA VYOMBO NJE
Next articleHAZINA SACCOS YATOA VITI MWENDO 15 BMH

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here