Home MICHEZO MWAKAGENDA CUP YAZINDULIWA KUKEMEA UKATILI, KUTUNZA MAZINGIRA

MWAKAGENDA CUP YAZINDULIWA KUKEMEA UKATILI, KUTUNZA MAZINGIRA

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Sophia H. Mwakagenda ameanzisha shughuli za michezo kwa kuandaa ligi yenye lengo la kuibua vipaji na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kulinda utamaduni wa kitanzania.

Shughuli za michezo zinafanyika katika uwanja wa Tandale Tukuyu mjini zikikutanisha timu kumi za Wilayani humo ili kuwakutanisha pamoja vijana na kuwahimiza kujikita kwenye shughuli za michezo na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Wachezaji na viongozi wao wanasema wamejiandaa kushiriki ipasavyo michezo hiyo ili kuboresha afya zao, kujiajiri na kuachana na makundi yasiyofaa wakijikita kwenye michezo.

Hata hivyo wamemshukuru Mbunge Sophia Mwakagenda kwa kuandaa ligi hiyo ambayo mshindi atatwaa ng’ombe mwenye thamani ya shilingi Million moja.

Mratibu wa ligi hiyo ya Mbunge Sophia Mwakagenda (Mwakagenda Cup) Abraham Nzunda anasema shauku yao ilikuwa kuandaa ligi itakayohusisha timu za Wilaya nzima ya Rungwe lakini wameanza na timu kumi ili kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana na kuimarisha afya zao.

Nzunda anasema pia lengo la kuwakutanisha pamoja wana Michezo hao ni kuhamasisha utunzaji wa mazingira ili kuhifadhi uoto wa asili na kuhimiza kulinda maadili ya kitanzania.

“Pia lengo lingine kubwa ni kukemea ukatili wa kijinsia, kulinda vyanzo vya maji, kutunza maadili ya kitanzania mfano kwa miaka ya sasa kumeibuka wimbi la ndoa za jinsi moja (ushoga na kusagana) na kulunda mazingira yetu”, Abraham Nzunda, Mratibu wa Mwakagenda Cup 2023.

Pia amewaasa vijana kutumia fursa hiyo kushiriki kwenye michezo hiyo ili kuimarisha afya zao akisema michezo ni ajira, ni afya na ni undugu.

Mbunge wa Viti maalumu kutoka wilayani Rungwe Sophia Hebron Mwakagenda ameanzisha mashindano hayo ili kuibua vipaji vya michezo, kuhamasisha uhifadhi wa mazingira ili kutunza uoto wa asili na kuhimiza utunzaji maadili na malezi bora katika jamii hasa kukemea vitendo vya ukatili ikiwemo kwa wanawake na watoto.

Previous articleWAZIRI MAJALIWA ACHARUKIA WATUMISHI 13 WA ARDHI, ASIMAMISHA WAWILI MWANZA , 11 KUREJESHWA DODOMA _ MAGAZETINI LEO JUMATANO OKTOBA 04/2023
Next articleMBUNGE WA MSALALA ASISITIZA KUENDELEA KUINUA SEKTA YA MICHEZO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here