Home KITAIFA MVUA ZA MARA KWA MARA KIKWAZO UTEKELEZAJI MRADI WA TANGA-PANGANI (KM 50)

MVUA ZA MARA KWA MARA KIKWAZO UTEKELEZAJI MRADI WA TANGA-PANGANI (KM 50)

Mradi wa Tanga – Pangani (km 50) unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja (100%), kumekuwa na mvua kubwa za mara kwa mara katika eneo la mradi, mabadiliko ya hali ya hewa hasa uwepo wa mvua nyingi umekuwa ukizuia shughuli za ujenzi kuendelea kama ilivyopangwa, Mkandarasi ameomba nyongeza ya muda ili aweze kukamilisha kazi ambapo kwa sasa Mkandarasi amepewa nyongeza ya muda wa matarajio (Interim Extension of Time )ya miezi mitatu (3) hadi tarehe 24 Agosti 2023.

Eng: Rwekiza ameongeza kuwa ujenzi wa tuta la barabara umekamilika kwa 75%, Magari yameruhusiwa kwenye baadhi ya maeneo kupita  juu ya tuta la barabara mpya inayojengwa kwa kuwa maeneo hayo awali yalikuwa na madaraja madogo ambapo huwa yanazidiwa na maji na kufanya yasipitike, Magari yakisha pita sehemu za madaraja Mapya makubwa hurejea kwenye njia ya mchepuko, na kwamba tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha hakuna uharibifu kwenye barabara mpya na endapo uharibifu utatokea basi Mkandarasi atarekebisha kwa gharama zake mwenyewe.

Aidha, barabara hiyo ni kiunganishi cha nchi za Kenya na Tanzania upande wa Pwani ya Afrika Mashariki na ikikamilika itachochea ukuaji wa uchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa usafiri, urahisishaji wa kufanya biashara na kuwezesha wananchi kuchangamana kwa urahisi, kuwezesha kufikika kwa urahisi kwenye vituo vya utalii na kuwa kiungo kizuri cha bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa na kuchochea uchumi wa Bluu.

Previous articleDC ILEJE AFUNGA MAFUNZO YA SKAUTI AWAACHA NA UJUMBE WA KUPINGA UKATILI
Next articlePROF. MKENDA: SERIKALI YATUMIA ZAIDI YA MILIONI 334 KUWAWEZESHA WANAFUNZI 122 WENYE MAHITAJI MAALUM

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here