Ametoa salaam hizo Aprili 26, 2023 wakati wa maadhimisho ya Kilele cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika Kimkoa Wilayani Mkuranga.
Ameeleza kauli mbiu ya mwaka huu ni Umoja na mshikamano ndiyo nguzo ya kukuza Uchumi. Ameeleza kikubwa katika Umoja ni kukuza Uchumi. Ameeongeza kuwa Muungano huo ni zao la vyama vyetu vya siasa ya TANU na ASP.
Mhe. Kunenge ameeleza kupitia wiki ya maadhimisho haya ya miaka 59 wakazi wa Mkoa wa Pwani wamejifunza kuwa waasisi wetu wa Muungano hakuwa wabinafsi waliweka maslah binafsi pembeni na kutaka Maendeleo.
Ameeleza shughuli mbalimbali zimefanyika katika wiki hii ya Muungano ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira, Kongamano la Muungano na Uzinduzi wa miradi ya Maendeleo.
Ameeleza Changamoto za Muungano zilizobaki ni chache na zinazidi kufanyiwa kazi.