Home KITAIFA MUUGUZI KCMC AUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI UCHOCHORO WA...

MUUGUZI KCMC AUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI UCHOCHORO WA MALINDI

Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Muuguzi wa hospitali ya KCMC Moshi Khudheifa Changa (26).

Akitoa taarifaa hiyo kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Simoni Maigwa amesema kuwa walio kamatwa ni watuhumiwa watatu wanaume na wanawake wawili (majina yao

yamehifadhiwa kwa sababu wengine wanaendelea kutafutwa) kwa tuhuma za kusababisha mauaji ya mfanyakazi huyo tukio lililotokea mtaa wa Malindi, kata ya Mawenzi, wilaya ya Moshi Manispaa usiku wa kuamkia Julai 2, 2023.

Kamanda Maigwa amedai kuwa siku ya tukio hilo marehemu alikuwa akipita eneo hilo kwenye njia ya uchochoro ndipo alipo vamiwa na watu hao kwa nia ya kumpora mali alizonazo.

“Katika purukushani hizo marehemu alijeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye mbavu upande wa kushoto usawa wa moyo na kupelekea kifo chake papo hapo.” alisema Kamanda Maigwa.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema lilifanikiwa kupata taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao walitoweka baada ya kutenda unyama huo ambapo Watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Rufaa KCMC Moshi kwa uchunguzi zaidi

Previous articleMRADI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU WATOA MAFUNZO KWA VIJANA GEITA JUU YA MBINU ZA KULINDA AMANI
Next articleWAKULIMA WATAKIWA KUTUNZA CHAKULA MARA BAADA YA MAVUNO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here