Mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge La Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania David Kihenzile, Mei 28, 2023 amekabidhi zawadi ya ng’ombe wawili, mmoja kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani na ng’ombe wa pili ikiwa ni zawadi kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo.
Katibu Mkuu Chongolo amepokea ng’ombe hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika wilaya ya Mufindi kata ya Nyololo Ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Iringa.
Lengo la kutoa zawadi hiyo ni kama neno la shukrani Kwa Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa na nyingi alizoweza kuzifanya na kuzitekeleza katika nchi kwa ujumla hasa jimbo la Mufindi Kusini kwenye sekta mbalimbali kama vile ujenzi wa majengo mapya ya madarasa sambamba ukarabati katika shule za msingi na sekondari, ujenzi wa hosptali ya wilaya, ujenzi wa barabara za lami, sambamba na uboreshwaji wa barabara zilizokuwa zimechakaa pia kuboresha katika sekta ya maji pamoja na nishati kwa baadhi ya vijiji vilivyopo jimboni hapo
Pia mbunge Kihenzile aliongezea kwa kusema
“Zawadi hizi zimetolewa na wanamufindi Kusini na mimi ninazikabidhi kwa niaba ya kuwawakilisha wananchi wa Mufindi Kusini kadhalika wamenituma niwasilishe salamu nyingi kwa Rais Samia na pongezi kwa kazi kubwa na nzuri zenye msingi wa kujenga na kuboresha Taifa Bora” alisema mbunge huyo