Home KITAIFA MTUMISHI KILOSA AUWAWA KIKATILI NYUMBANI KWAKE NA WASIOJULIKANA

MTUMISHI KILOSA AUWAWA KIKATILI NYUMBANI KWAKE NA WASIOJULIKANA

Mtu mmoja aliyefahamika kwa Merisiana Temu (42) mtumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ameuawa kwa kukatwa sehemu ya shingoni nyumbani kwake mtaa wa Mamboya Manzese kata ya Mkwatani Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro.

Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba amesema,taarifa za kuuawa kwa mtumishi huyo walizipata majira ya saa nne usiku Julai 17 mwaka huu baada siku hiyo kutoonekana kazini bila ruhusa na simu yake ikiwa haipatikani

Mabuba amesema baada ya kutoonekana kazini Julai 17 mwaka huu ndipo watumishi wenzake majira usiku walifika nyumbani kwake kwa lengo kufuatilia kujua kilichomsibu marehemu kutofika kazini ndipo walikuta mlango ukiwa wazi na funguo zipo kwa ndani na walipoingia sebuleni wakakuta amelala chini damu nyingi zikiwa zimemwagika chini huku akiwa na majeraha sehemu mbalimbali.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa Morogoro ACP Hassan Omary ,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema marehemu alikua akiishi peke yake hadi sasa chanzo cha tukio hilo hakijafahamika huku Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kusisitiza kamati ya ulinzi na usalama kuendelea kuchunguza aliyehusika na tukio hilo

Previous articleNAIBU WAZIRI NDERIANANGA AKEMEA UNYANYAPAA KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI -WAVIU
Next articleAWESO AMUONDOA MKANDARASI MRADI WA MAJI KAZURAMIMBA; AAGIZA MWEZI MMOJA WANANCHI WAPATE MAJI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here