Home MICHEZO MSHINDANO YA GOFU YAMEANZA RASMI MOROGORO

MSHINDANO YA GOFU YAMEANZA RASMI MOROGORO

Mashindano ya wazi ya mchezo wa Gofu yameanza rasmi mkoani Morogoro yakihusisha washiriki 121 kutoka klabu mbalimbali za mchezo huo ikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya na Zambia.

Club ya Morogoro Gymkhana ndio waandaaji wa mashindano ya wazi ya mchezo wa gofu 2023 wakishirikiana na Chama cha Gofu Tanzania TGU ambapo mchezo wa utangulizi ukihusisha washiriki 21.

Kufuatia mashindano haya katibu chama cha Gofu Tanzania Enock Magire amesema,kukosekana kwa vijana wanaoshiriki mchezo huo umepunguza idadi ya wachezaji wa kulipwa huku akitoa ombi kwa wizara ya michezo kutupia jicho mchezo huo

Kwa upande wake Angel Eaton miongoni mwa washiriki wa kike amewasihi vijana wakike kujitokeza kushiriki mchezo huo .

Previous articlePROF JANABI ATOA USHAURI KWA KLABU ZA LIGI KUU
Next articleRC MAKALLA ATAKA ELIMU ZAIDI ITOLEWE KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here