Home KITAIFA MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE WAFIKIA ASILIMIA 90.19

MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE WAFIKIA ASILIMIA 90.19

 

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Maharage Chande amesema utekelezaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha umeme wa kiasi cha megawati 2,115 hadi kuisha mwezi huu wa Agosti utakuwa umefikia asilimia 91.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 25/2023 wakati akiwa ziarani kuangalia maendeleo ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Maharage Chande amesema mpaka sasa Maendeleo ni mazuri na matarajio yao hadi kufikia Juni 2024 wanaweza kutoa umeme wa kwanza.


“Maendeleo ya mradi wa Mwalimu Nyerere ni mazuri sana mpaka mwezi Julai tulikuwa tumefika asilimia 90.19 hivi na tunategemea mwezi huu wa Agosti ukiisha tutaingia asilimia 91….Tayari hapa tumeshaleta wafanyakazi zaidi ya 20 na tutaenda kwa makundi makundi wakianza kujiandaa kuendesha mradi pale utakapokamilika kwa hiyo wakati zikiwa zimebaki hizi asilimia 10 tunaanza kuandaa watu wetu kwa uendeshaji wa mradi huu. Kwa hali ilivyo dalili zote zinaonyesha kwamba tunaweza kufanikiwa kuutoa umeme wa kwanza Juni 2024 kwani kazi kubwa iliyobaki sasa ni ya kufunga mitambo ambayo inaendelea vizuri.”_ Alisema Maharage

Chande amesema kukamilika kwa mradi wa Bwawa la (JNHPP) utaleta afueni kubwa kwani kuanzia mwaka jana hadi mwaka huu ongezeko la mahitaji ya juu ya umeme ni zaidi ya megawati 100 kutokana na shughuli za uchumi.

“Kama mnavyofahamu mwaka jana mahitaji ya juu kabisa ya umeme yalikuwa kwenye kama megawati elfu moja 354 hivi na nukta chache lakini tarehe 17 /8/2023 tumeweka rekodi nyingine ya mahitaji ya juu kufika megawati elfu 482.7 kwa hiyo utaona kuanzia mwaka jana mpaka mwaka huu ongezeko la mahitaji ya juu ni zaidi ya megawati 100 kwa hiyo kuna mashindano makubwa yakutumia umeme yanaongezeka kutokana na shughuli za uchumi na sisi tunashindana kuongeza umeme zaidi ili uweze kukidhi mahitaji ya uchumi kwa hiyo ukamilikaji wa mradi huu utatuwezesha kuhakikisha mashindano hayo tunashinda kwa kuwa na umeme zaidi kukidhi mahitaji ya uchumi” Alieleza Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo amesema huenda miaka ya usoni tatizo la umeme likawa historia nchini Tanzania kutokana na Mradi huo wa umeme wa Mwalimu Nyerere

“Mtakumbuka tuliongeza kituo cha Kinyerezi (I) ambacho kilikuwa na megawati 185 lakini kwa ukuaji huu kimeshamezwa tayari umeme ule unatumika lakini tunaimani kwamba kukamilika kwa mradi wa Mwalimu Nyerere pengine itakuwa mwisho wakuwa na upungufu wa umeme ambao mara nyingi tumekuwa tukiupata kwenye miezi ya 10-11 -12 wakati kunakuwa na hali ya maji kushuka. Leo tunafaraja kwamba mradi unakwenda vizuri na pengine mambo ya upungufu wa umeme yakawa ni historia kwa miaka ya usoni.”_Alisema Mkurugenzi Mtendaji Tanesco


Akizungumza hali ya ujazo wa maji katika Bwawa la JNHPP amesema hadi kumfikia leo Agosti 25 /2023 kimo cha maji cha bwawa kimefikia mita 164.6.

“Mpaka siku ya leo tupo ujazo mita 164.6 na maji yanayotosha kuzalisha umeme ni mita 163 kwa hiyo kama tungekuwa tumemaliza kufunga mashine tungeweza kuzalisha umeme na bwawa hili ni kimo chake ni mita 184 kwa hiyo hali inakwenda vizuri tukipata mvua itakwenda vizuri zaidi ndio maana tunaomba zije mvua za heri mvua za kiasi zisizoleta athari kwenye mradi”_ Alisema Chande


Aidha Mkurugenzi Maharage ametoa ufanunuzi juu ya swala la kuwa na unafuu wa bei ya umeme pindi bwawa hilo litakapomalizika nakusema ;

“Kama tulivyosema bwawa letu limefanikiwa asilimia 90.19 nadhani kwa wakati huu Watanzania na wateja wetu wanachotaka kusikia kwa sasa ni mradi unakwenda je? kwa sasa ni sisi Umakini mawazo akili yetu nikatika kumaliza mradi maswala ya bei ni maswala mepesi na ni maswala ya mazungumzo sasa hivi maswala ya site ni kazi na tutajikita kufanya kazi ili miradi uweze kukamilika juni 2024” alisisitiza

 

Previous articleFIFA YAANZA UCHUNGUZI KUHUSU TUKIO LA RAIS WA SOKA UHISPANIA KUMBUSU MCHEZAJI
Next articleWAZIRI BALOZI DKT. PINDI CHANA AFUNGUA TAMASHA LA PILI LA UTAMADUNI, NJOMBE YANEEMEKA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here