Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Peter Msigwa akiongozana na viongozi mbali mbali amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliwa halmashauri ya mji wa Njombe uliojengwa kwa nguvu za wananchi ulioghalimu zaidi ya shilingi milioni 12 unaonufaisha kaya 150 za vitongoji vya Itowa na Canada.
“Mmefanya kazi ya serikali kwa hiyo viongozi wenu wasikie kwamba mmefanya majukumu ambayo serikali ilipaswa kuyafanya,nyumba 150 sio haba na kwa hili tunaiambia serikali uwezekano wa kupata maji safi na salama upo”_Peter Msigwa
Awali mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe Rose Mayemba amesema wananchi wa kijiji hicho waliamua kutengeneza mradi wao ili kufikisha maji kwenye makazi kutokana na kukosa huduma hiyo licha ya kuwa na vyanzo vya maji karibu ambapo mpaka sasa kaya 405 bado hazijafikiwa na mradi.
Emmanuel Mgulo kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Uliwa amesema mradi huo umetekelezwa kwa takribani mwaka mmoja ambapo ulianza Desember 26,2022 na kukamilika February 5,2023 kutokana na fedha zilizopatikana kutoka kwa wananchi kwa njia ya uchangishaji.