Home KITAIFA MRADI WA DIGITAL TANZANIA KUSAIDIA KUPUNGUZA GHARAMA ZA INTANETI

MRADI WA DIGITAL TANZANIA KUSAIDIA KUPUNGUZA GHARAMA ZA INTANETI

 

‘π™ˆπ™§π™–π™™π™ž 𝙬𝙖 β€˜π˜Ώπ™žπ™œπ™žπ™©π™–π™‘ π™π™–π™£π™―π™–π™£π™žπ™–β€™ unatarajiwa kuimarisha utoaji wa huduma kwa njia ya kidijitali kati ya Serikali, Wananchi pamoja na Wafanyabiashara sambamba na kuchochea uwekezaji katika miradi ya kidijitali nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Eng. Benedict Ndomba alipozungumza na mwandishi wetu kuhusu mradi huo ofisini kwake jijini Dodoma.

Alibainisha kuwa, mradi huo una malengo makuu mawili ambayo ni kuongeza upatikanaji wa huduma za mtandao wa intaneti zenye gharama nafuu na ubora wa juu kwa serikali, wafanyabiashara na wananchi sambamba na kuboresha uwezo wa serikali wa kutoa huduma za umma kidijitali.

β€œLengo la pili la mradi huo ni kuchangia upatikanaji wa intaneti na upatikanaji wa huduma za umma kidijitali ili kuwezesha sekta binafsi kuwekeza katika miradi ya kidijitali na kuongeza ajira”, alisema Ndomba.

Kupitia mradi huo e-GA inayo majukumu matatu ambayo ni upanuzi wa mtandao wa serikali, uboreshaji wa vituo vya kuhifadhia data pamoja na masafa ya intaneti β€˜bandwith’, ambapo kupitia mradi huo jumla ya vituo 660 vinatarajia kunufaika.

Mei 23, mwaka huu Wawakilishi wa Benki ya Dunia wanaosimamia mradi huo pamoja na wajumbe wa kamati hiyo walikutana ofisi za e-GA Mtumba jijini Dodoma na kufanya kikao cha majadiliano juu ya mradi huo ambao utekelezaji wake unaendelea.

Mradi wa β€˜Digital Tanzania’ unaofadhiliwa na benki ya Dunia unatekelezwa kwa usimamizi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Pamoja na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zinazohusika na TEHAMA ikiwemo e-GA.

Previous articleZITTO ACHANGIA UJENZI MSIKITI WA WILAYA TANDAHIMBA
Next articleNAIBU WAZIRI KHAMIS AHIMIZA WADAU KUENDELEA KUTOA ELIMU YA MAZINGIRA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here