Mpishi Hilda Bassey Effiong maarufu kama Hilda Bacci amekuwa maarufu mtandaoni baada ya kupika bila kukoma kwa zaidi ya saa 90, katika jaribio lake la kuvunja rekodi ya dunia.
Hilda Raia wa Nigeria akiwa mbele ya umati wa watu ametumia zaidi ya sahani 100 tofauti tangu kuwasha jiko lake saa tisa mchana siku ya alhamisi ya wiki iliyopita.
Rekodi ya sasa iliyonakiliwa na Guiness ni ya saa 87 na dakika 45 iliyowekwa na mwanamama Lata Tondon wa huko Riwa katikati ya Taifa la India mnamo mwaka 2019.
Bacci mwenye umri wa miaka 27 awali alipanga kupika kwa saa 96 pekee – Hadi jana jumatatu lakini umati uliokuwa ukimshuhudia ukumbini ulimtaka afikishe saa 100.